Intro
Kwenye tutorial hii ntawaonyesha jinsi ya kuinstall ubuntu katika kompyuta yako. Kwa wale wenzangu wasiofahamu ubuntu ni nini?. Ubuntu ni operating system kama ilivyo microsoft windows nadhani wengi tutakuwa tunaifahamu ila yenyewe imetokana na linux. Angalia tutorial yangu ya linux na distro mbali mbali ili ufahamu vizuri kuhusu linux.Kwa nini ubuntu?
Najua wengi mtakuwa mnajiuliza kama kompyuta yangu imekuja tayari ina microsoft windows kwa nini niinstall ubuntu. Kwanza kabisa ubuntu itafanya kompyuta yako ifanye kazi kwa haraka zaidi kushinda microsoft windows, nani asiyetaka kubonyeza program fulani na hapo hapo ikafunguka? Kama unahisi unahitaji kompyuta yako iwe na spidi zaidi basi ubuntu itakufaa. Sababu ya pili ni kwamba kwenye ubuntu hamna virusi, kwa sababu hiyo basi hautakuwa na haja ya kutafuta antivirus au kuhofu labda siku mafile fulani yatakuwa corrupted(yataharibika). Sababu ya tatu ni urahisi wake wa kuinstall kwani unaweza kuinstall kwa kutumia flash disk ambayo ni njia ya haraka zaidi na kama una zile kompyuta ndogo (minicomputer) ambazo hazina CD/DVD drive basi hautahitaji kununua external CD/DVD drive. Sababu ya nne ni kwamba ubuntu haitumii space/memory kubwa kwenye kompyuta yako, file lake la kuinstalia lina ukubwa wa chini ya 700MB kwa hiyo unaweza kutumia CD na sio DVD kama microsoft windows 7, amabayo inachukua memory zaidi ya 2GB. Naona nimeleta longo longo nyingi, hebu tuchape kazi.Jinsi ya kuinstall step by step
1. Andaa flash disk yako au CDKwanza kabisa utahitaji kudownlaod file la kuinstalia(ISO file au image file), unaweza kulipata kutoka hapa. Bonyeza start download. Kama unafahamu vizuri kompyuta yako ni 32bit au 64bit changua kutoka kwenye "Choose your flavour", kama huulewi chochote basi bonyeza start download, Usihofu kwani file utakalolipata ndio ubuntu wanalirecommend kutumia. Ukishamaliza kudownload burn hilo file kwenye CD/DVD kwa kutumia program yoyote ya kuburn kama nero, free iso burner. Unaweza pia kuburn kwenye flash disk yako, kama unataka kutumia flash disk soma "Jinsi ya kuburn ubuntu kwenye flash disk". Ukishamaliza kama unatumia flash disk ichomeke kwenye kompyuta yako na kama unatumia CD/DVD basi iweke kwenye CD/DVD drive halafu restart kompyuta yako.
2. Maandalizi kabla ya kuinstall
Kompyuta wakati inajiwasha itatafuta kama kuna CD/DVD au flash disk, ikiona ni bootable itaanza kuzisoma. Muda mwingine inawezekana boot sequence ya kompyuta haianzi na CD kwa hiyo kompyuta haitaisoma CD na utashindwa kuinstall, inabidi ubadilishe boot sequence kwenye boot menu kwa kushikilia(hold) F2 wakati kompyuta inawaka. kompyuta zingine hazitumii F2, kwa hiyo ni vyema kuangalia screen ya kompyuta yako wakati inawaka kwani huwa inaandika ubonyeze kitufe gani ili boot options zitokee. Vitufe vinavyotumika na kompyuta nyingi huwa ni F1, F2, F12, ESC, au backspace. Ukishaseti save and exit. Sasa kompyuta itaweza kuisoma CD/DVD au flash disk. Cha kuzingatia ni kwamba chochote utakachotumia iwe CD au flash disk lazima kiwe cha kwanza kwenye boot order. kompyuta ikishamaliza kusoma utaona screen hiyo hapo chini, Chagua lugha upande wa kushoto halafu bonyeza install ubuntu. unaweza kubonyeza try ubuntu, ili utumie ubuntu bila kuiinstall!
Kama hauna internet au internet yako ipo slow usitick download updates while installing. Bonyeza continue.
Kama unatumia windows ni vizuri kuchangua install ubuntu alongside windows. Hii itafanya windows yako isifutwe na uweze kutumia zote kwa pamoja. Bonyeza continue.
Shikilia katikati ya windows na ubuntu ili kuchagua kiasi cha memory utakachotumia kwa ajili ya ubuntu. Bonyeza Install Now.
3. Anza kuinstall
Baada ya kubonyesha install now, step zinazofuata ni kujaza maswali sehemu zitakazohitajika, ubuntu itaendelea kujiinstall wakati wewe unaendelea kujaza. Kwenye screen hiyo hapo chini chagua sehemu ulipo, unaweza ukaandika au ukabonyeza kwenye ramani. Kisha bonyeza Continue.
Chagua keyboard style yako,kama upo bongo keyboard nyingi zinakuwa ni English(US), kama una aina tofauti pia unaweza kuichagua, kisha bonyeza Continue.
Ingiza jina na password unayotaka kutumia, kama hupendi kutumia password wakati kompyuta inawaka chagua Login automatically. Kisha bonyeza Continue.
Mpaka hapo utakuwa umeshamaliza kujaza maelezo yanayohitajika, sasa unaweza kusubiri ubuntu imalize kujiinstall.
Ikishamaliza itakuomba kurestart, bonyeza Restart Now, kompyuta ikishawaka itakuwa tayari, na unaweza kuanza kuifurahia ubuntu!
Links
Ubuntu setup file -- Bonyeza Hapa!Jinsi ya kuburn ubuntu kwenye flash disk -- Bonyeza Hapa!