Tuesday, October 9, 2012

Jinsi ya kutumia gcc compiler(Basic)

Intro

Kwenye tutorial hii ntawaonyesha jinsi ya kutumia gcc compiler kucompile programs zako. Kwa kirefu gcc inamaanisha GNU Compiler Collections ambayo inajumuisha programming language nyingi kama vile C/C++, Java, Objective-C na zinginezo nyingi. Kwenye hii tutorial ntawaonyesha jinsi ya kucompile C/C++ programs, kwa lugha nyingine kama java na objective-c jinsi ya kucompile kunafanana utahitaji kuongeza vitu vichache tu. Ili kufuatisha vizuri hii tutorial inabidi uwe kwenye linux na uwe umeinstall gcc.


Jinsi ya kuinstall

Kwa wale wanaotumia Ubuntu au Debian-based distro yoyote ya linux watatumia commands zifuatazo. Fungua terminal, shikilia Ctrl+Alt+T.
sudo apt-get update
sudo apt-get upgrade
sudo apt-get install gcc build-essential
au hivi kama kuna version maalum ambayo unataka kuinstall. kwenye gcc-4.4 badilisha weka version unayoitaka.
sudo apt-get install gcc-4.4

Jinsi ya kucompile

Kwa ufupi
Kwanza kabisa inabidi uwe upo kwenye directory ambayo source files zako zipo, tumia commands (cd, ls) kwenda kwenye hiyo directory. cd kwakirefu ni "change directory" inatumika kubadili directory, na ls kwa kirefu "list" inatumika kulist directories na files ambazo zipo kwenye current directory.
kwa mfano
mkdir source
cd source
N.B: mkdir kwa kirefu ni "make directory" inatumika kutengeneza directory, baada ya hii command ukiandika ls, itakulistia directories na files zote kwenye current folder. folder na directory zinamaanisha kitu kimoja

kwa ufupi tu, kama unataka kutumia program yoyote kwa kutumia commands kwenye terminal basi inabidi uandike jina la hiyo program ikifuatiwa na inputs ambazo hiyo program inahitaji. Jinsi ya kuweka inputs kwenye program inategemea sana na programmer aliyeiandika hiyo program lakini kwa linux syntax inakuwa hivi

jina-la-program  -label1 input1 -label2 input2 ...

labels zinakuwa zinaonyesha hiyo input inayokuja inamaanisha nini au muda mwingine inatumika kuchagua program ifanye kitu gani baina na vitu vingi. Labels huwa zinaandikwa kwa kuanza na dash(-). Mara nyingi labels zikiwa ni herufi moje zinaanziwa na dash na zikiwa ni herufi zaidi ya moja zinaanziwa na dash mbili(--). kwa mfano, gcc -Wall main.c -o main . gcc ni jina la program ambayo ni compiler, -Wall ni label imetumika kuswitch warnings zote ambayo compiler itatoa ziwe displayed wakati wa kucompile, -o ni label inaonyesha file linalokuja ni jina la output file. kwa hiyo hii command itacompile main.c na kutoa program ambayo itaipa jina la main, unaweza kubadilisha jina la kwenye -o, sio lazima yafanane.

N.B: gcc au g++ inadetect source files automatically kwa hiyo haina haja ya labels kwa ajili ya input source files. Pia hauhitaji kuandika header files(.h files).

Simple
Kama una file moja tu, mfano main.cpp na kwenye hilo file hamna libraries zozote unazozitumia zaidi ya standard libraries, andika

g++ main.cpp -o main 

hii command inachukua main.cpp kama input na kuicompile na kutoa main program. -o inamaanisha jina la output file.

Kucompile program ambayo source files zake zipo kwenye folder moja
Kwa programs ambazo source files zipo kwenye folder moja syntax ipo hivi

g++ list-of-all-input-files -o program-name

mfano:
g++ source1.cpp source2.cpp source3.cpp -o myprogram

Kwa wale ambao ndio wanaanza kujifunza C au C++ programming hii tutorial inawatosha, Ila pia unaweza kuendelea na tutorial "Jinsi ya kutumia gcc compiler(Advanced)"

0 comments:

Post a Comment