Tuesday, October 16, 2012

Jinsi ya kuandaa bootable USB flash disk ya windows 7

Intro

Katika tutorial hii ntawaonyesha jinsi ya kuandaa bootable flash disk yenye windows 7 kwa wale wanaotaka kuinstall windows 7 kwa kutumia flash disk. Kama ulishawahi kujiuliza kwa zile computer ambazo hazina CD/DVD drive inakuwaje watu wanainstall operating sytems, basi hii ni njia mojawapo na rahisi. Unaweza pia kununua external CD/DVD drive ambayo inachomekwa kwenye USB, lakini kwa nini ufanye hivyo wakati unaweza kuifanya flash disk yako ikainstall windows. Leo ntawaonyesha kufanya hivi wakati unatumia ubuntu. Kwa wale ambao wanatumia windows, zipo programs nyingi kwenye internet kwa ajili ya kazi hii, zikiwemo za bure na kulipia. Baada ya longo longo wacha tuchape kazi.


Jinsi ya Kuandaa

Kwanza kabisa utahitaji program inaitwa WinUSB, Fungua terminal(Shikilia Ctrl+Alt+T). kisha andika commands zifuatazo moja baada ya nyingine.
sudo add-apt-repository ppa:colingille/freshlight
sudo apt-get update
sudo apt-get install winusb
Kwa wale wasiofahamu commands za ubuntu, apt-get inatumika kuinstall, kuondoa program yoyote, ina kazi nyingine pia. Sudo ikiwa kabla ya command yoyote inamaanisha "command inayofuata irun kama root(administrator kwa windows)".

Ukishamaliza program itajiinstall kwenye system tools(ndani ya Applications). ifate na uibonyeze. Chagua file lako la ISO, chomeka USB flash disk yako. Flash disk itaonekana kwenye Target device baada ya kuichomeka. Hakikisha kwenye flash disk yako hamna kitu cha muhimu kwani hii program itaiformat flash disk. Ukisha chagua flash disk kwenye Target device bonyeza install, kisha subiri program ifanye kazi yake. Baada ya kumaliza flash disk yako itakuwa tayari kwa matumizi.


Hii program pia inarun kwa command lines kwa wale wanaopenda commands. Kwenye terminal andika winusb au winusb --help , utaona maelezo ya jinsi ya kutumia.



0 comments:

Post a Comment